School Start Date and Return to Learn Plan - Swahili

August 26, 2020 08:20 PM
CRCSD_vertical.cmyk.tag

Ndugu Familia,

Tunahabari njema za kuwajulisha! Shule zitaanza siku ya Jumatatu, Septemba 21.

Shule zetu nyingi zimeharibiwa vibaya ba kimbunga cha Derecho. Kutokana na uhalisia wa uharibifu wa majengo na umeme/mtandao katika mji wetu, timu yetu imekuwa inafanya kazi kuandaa utaratibu utakatuwezesha kufuata mpango wetu wa awali tuliopendekeza wa kuanza shule madarasani na kwenye mtandao.

Barua pepe hii ina maelezo ya utaratibu wetu, lakini kitu kikubwa tungependa ujue:

  • Masomo ya CRCSD yataanza Septemba 21, 2020.
  • Wanafunzi wa shule za msingi watahudhuria madarsani au mtandaoni kwa kutegemea walivyochagua kwanzoni mwa mwezi huu.
  • Wanafunzi wote wa Middle School  na High School watasoma kupita mtandaoni pekee( hata kama walichagua kuhudhuria masomo darasani mwanzoni mwa mwezi) isipokuwa shule ya Metro ambayo itakuwa na wanafunzi waliochagua kuhudhuria madarasani.
  • Kuna majengo 18 yaliyopo kuhudumia wanafunzi washule za msingi waliochangua kuhudhuria madarasani, wenye mahitaji makubwa zaidi, na wanafunzi na wafanyakazi wasiokua na mtandao.
  • Pale matengenezo yatakapokamilika majengo mengine yatafunguliwa kwa wanafunzi khudhuria madarasani katika kipindi cha muhula wa pili wa mwaka wa masomo.
  • Kalenda yam waka wa masomo itabaki kama awali, ambapo Juni 21, 2021, kama siku ya mwisho ya mwaka wa masomo.

Kama ilivyopangwa chini, tumetoa kipaumbele kwa makundi mawili ya wanafunzi:

  • Wanafunzi wa Chekechea na Msingi wamepewa kipaumbele kutokana na mahitaji yao ya ukuaji na kwasababu majengo yao mengi yameharibika kwa kiasi kidogo; na
  • Wanafunzi wetu wa elimu maalumu wanamahitaji makubwa.

Shule za Msingi------

Shule zifuatazo zitaanza masomo madarasani na mtandaoni siku ya Septemba 21:

Arthur                                                              Cleveland

Coolidge                                                          Erskine

Grant Wood                                                    Harrison

Hiawatha                                                         Jackson

Johnson Steam Academy                              Cedar River Academy at Taylor

Madison                                                          Truman

Van Buren                                                       Viola Gibson

Wright

 

Shule za msingi kwenye jedwali hapo chini hazitakua tayari kwa wiki chache. Wanafunzi katika shule hizo ambao wanapanga kurudi madarsani watahudhuria jingo la shule nyingine. Jedwali la shule za msingi na majengo mbadala ambapo watahudhuria mpaka pale ukarabati utakapokamilika mashule kwao. Wanafunzi kutoka hizo shule  ambao wamepanga kusoma mtandaoni wataendelea kufanya hivyo.

Shule Ya Msingi Shule Mbadala ambapo watahudhuria
Kenwood Harding Middle School
Nixon Harding Middle School
Hoover Roosevelt Middle School
Pierce Roosevelt Middle School
Garfield Wilson Middle School
Grant Wilson Middle School

 

Shule za Middle na High

Wanafunzi wote wa shule za Middle na High wataanza masomo kupitia mtandaoni. Pale matengenezo yatakapokamilika, wanafunzi watahudhuria madarasani kama walichagua hivyo katika dodoso la mwamzoni mwa mwezi huu. Shule pekee ambayo iko tofauti ni ile ya Metro. Shule ya Metrao High itakua na wanafunzi watakaoanza kuhudhuria madarasani kama familia zilichagua hivyo.

Kwa wanafunzi wote watakaosomea mtandaoni-----

Kimbuga kimeharibu miundombinu mingi ya intaneti kwenye mji wetu. Maandalizi maalum yamefanywa kwa familia zilizochagua kusoma mtandaoni lakini hazina intanet kwasababu ya kimbunga. Tutaandaa vituo vya intaneti kwenye baadhi ya mashule ya sekondari au majengo ya jamii ilikuahakikisha wanafunzi wote wanapata huduma. Kwa ziada, muunganisho wa intanet tayari umeshafanyika kwa wanafunzi/familia zenye vigezo kwa mujibu wa takwimu zaetu za Juni, 2020. Taarifa zaidi zitapatikana mapema iwezekanavyo kuhisina na hili.

Wakati naelewa kuwa ni memgi ya kutafakari, ningependa kuwajulisha  ili muelewe maamuzi magumu na ili isaidie kuwasaidia wanafunzi, kila mmoja wet una wale wote walioathirika katika kipindi hiki cha kipekee katika historia ya CRCSD. Tusaidiane wote ili tuvuke kwenye kipindi hiki kigumu.

Kwa mara nyingine tena, Asanteni sana kwa baraka zenu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Kila la Kheri
Noreen Bush
Superintendent

Back to news
Close